RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 30 Julai, 2021 ameongoza Watanzania katika mapokezi ya Ndege mpya aina ya Bonbadier Dash 8-Q400 na kisha kuizindua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kuwasili kwa Ndege hiyo iliyotokea nchini Canada kunaongeza idadi ya Ndege zilizonunuliwa na kuwasili kufikia 9 kati ya 11, Ndege nyingine 2 zinatarajiwa kuwasili mwezi Oktoba 2021.
Akizungumza wakati wa hafla ya kupoka Ndege hiyo, Mhe. Samia amesema usafiri wa anga ni kichocheo muhimu cha maendeleo duniain kwa sababau usafiri huo ni wa haraka, salama na wenye kutumiwa na watu wengi.
Mhe. Rais Samia amesema mbali na usafiri wa anga kusafirisha watu, pia ni muhimu katika kusafirisha bidhaa mbalimbali hususani zinazoharikiba haraka kama vile matunda, mbogamboga, samaki, maua, nyama na nyinginezo.
Amesema Serikali imeamua kununua Ndege ya kusafirisha mizigo kwa sababu nchi yetu ni mionognzi mwa wazalishaji wakubwa wa matunda, mbogamboga na maua ambapo mwaka 2019, Tanzania iliuza nje mazao yenye thamani ya takribani Dola za Kimarekani milioni 700 na inatarajia hadi kufikia mwaka 2025 kuingiza Dola za Marekani bilioni 2.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema ili nchi iweze kuvutia watalii wengi na kunufaika nao ni lazima iimarishe usafiri wa ang ana ndio sababu Serikali iliamua kufufua Shirika la Ndege la ATCL ikiwa na malengo ya kupokea watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025 katoka watalii milioni 1.5 mwaka 2019.
Amesema Serikali imeamua kuimarisha huduma za usafiri nchini ili iweze kunufaika na fursa za kijiografia za kupakana na nchi 8, ambapo kati ya hizo 6 hazina bandari.
Mhe. Rais Samia amezihimiza Wizara za Viwanda na Biashara, Wizara ya Uwekezaji na Sekta Binafsi kuweka mikakati ya kunufaika na fursa hizo ikiwemo kuanzisha kongani za kiuchumi kwenye maeneo ambapo miundombinu ya usafiri inajengwa.
Vile vile, Mhe. Rais Samia ameipongeza ATCL kwa kuimarika tangu ilipofufuliwa ambapo idadi ya watu wanaosafiri kwa Ndege za shirika hilo imeongezeka kutoka wastani wa abiria 4,000 hadi 60,000 kwa mwezi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi amesema ATCL imeongeza safari za kimataifa kutoka kituo kimoja cha Comoro hadi saba ambavyo ni Burundi, China, India, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Lubumbashi, Kalemie, Ndola, Nairobi, Dubai, Muscat na London.
Mapokezi ya Ndege hiyo mpya pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Pamella O’Donell, viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.