RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya Miradi ya Maji ya Miji 28 katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino.
Mikataba hiyo imesainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na makampuni ya JW INFRA Ltd, AFCONS Infrastructures Ltd, Larsen & Toubro, Megha Engineering and Infrastructures Ltd, China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na Jandu Plumbers Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ameitaja miji itakayonufaika na miradi hiyo kuwa ni Handeni, Korogwe, Muheza, Pangani, Kilwa, Masoko, Nanyumbu, Ifakara, Chunya, Rujewa, Wangingo’mbe, Makambako, Njombe, Kiomboi, Singida, Manyoni na Chemba.
Miji mingine ni Chamwino, Mugumu, Kasulu, Mpanda, Sikonge, Urambo, Kaliua, Kayanga, Geita, Chato, Mafinga pamoja na ukanda wa Makonde.
Utekelezaji wa Miradi hiyo ni asilimia 8 ya mikakati ya Serikali ya usambazaji wa huduma ya maji safi na salama maeneo ya mijini na vijijini.
Rais Samia amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji ili hadi kufikia mwaka 2025 huduma ya usambazaji wa maji safi na salama ifikie asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini.
Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara ya Maji kuisimamia vyema miradi hiyo ya maji pamoja na Wakandarasi wanaopewa kujenga ili iwe na manufaa kwa pande zote mbili.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.