RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na kuwa Utamaduni hutangaza mila na desturi za nchi lakini pia ni biashara na chanzo kikubwa cha mapato kwa sababu ni moja ya vivutio vya utalii.
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 08 Septemba, 2021 katika Viwanja vya Red Cross Kisesa, Magu Jijini Mwanza wakati akifungua Tamasha la Utamaduni lilioandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema Serikali imejipanga kupanua wigo wa vivutio vya utalii, ukiwemo utalii wa utamaduni ambapo tayari ameanza kuchua hatua za kutangaza vivutio vya utalii, biashara na uwekezaji kupitia filamu inayoendelea kurekodiwa katika kipindi maarufu cha Royal Tour.
Mhe. Rais Samia amewaomba Machifu hao nchini kwa kushirikiana na Serikali kudumisha amani na usalama ikiwa ni pamoja na kusuluhisha migogoro kwenye jamii zinazowazunguka.
Vilevile, Mhe. Rais Samia amewasihi viongozi hao wa kimila kuwahimiza Watanzania kujilinda na janga la UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na kupata chanjo.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewaomba viongozi hao wa kimila kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa litakalofanyika mwakani 2022.
Katika Tamasha hilo, Machifu wamemtawaza Mhe. Rais Samia kukwa Chifu Mkuu wa Machifu waote nchini na kuma jina la Chifu Hangaya likiwa na maana ya Nyota ya asubuhi inayong’aa.
Mara baada ya kutawazwa kuwa Chifu Mkuu Hangaya, Mhe. Rais Samia amewashukuru Machifu hao kwa heshima waliyompa na kuwaahidi kufanya kazi kwa bidi ili kuwaletea maendeleo Watanzania.
Mhe. Rais Samia mara baada ya kuhitimisha Tamasha hilo la Utamaduni amerejea Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.