• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia atoa Bil. 1.3 kukamilisha mradi wa maji Dodoma

Imewekwa tarehe: August 30th, 2021

SERIKALI imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 1.3 ili kukamilisha mradi wa maji kwa wakazi wa Njendengwa, Ihumwa, Nzuguni, Nyumba mia tatu, Iyumbu, Soko Kuu la Job Ndugai na FFU jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu tarehe 30 Agosti 2021 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Ihumwa Njedengwa wenye thamani ya Sh. bilioni 2.7.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA).

Waziri Aweso amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilion 1.3 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo na ununuzi na usimikaji wa pampu kubwa mbili za kusukuma maji.

Pia, ulazaji wa mabomba ya kupeleka maji kwenye tenki lenye urefu wa Km 11.6, ulazaji wa mabomba ya kusambazia maji yenye urefu wa Km 5.6 kwenda maeneo ya Iyumbu, Njedengwa na Mwangaza, Nyumba 300, FFU, Kituo Kikuu cha Mabasi, Soko Kuu la Job Ndugai na eneo la Nzuguni.

Aidha, Waziri Aweso amewataka DUWASA kuongeza nguvu mara moja pindi watakapopata fedha hizo ili kazi ikamilike ndani ya miezi miwili kuanzia sasa na wananchi waanze kupata maji.

Amesema awali serikali ilitoa shilingi bilioni 1.4 kwa lengo la kuyafanya Makao Makuu ya Nchi Dodoma kuondokana na changamoto ya majisafi ambayo ilikuwa ikiwakabili wananchi.

"Tunajua serikali inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ni serikali ambayo inawajali wananchi wa hali ya chini. Pamoja na kuwajali watu wa hali ya chini inakusudia kumtua mama ndoo kichwani," amesema Waziri Aweso

"Kwa maana hiyo mama yetu Samia ameona ni vyema kuwawezesha wakazi wa Dodoma ambako ni Makao Makuu ya Nchi, Shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika maeneo haya," amesema Waziri huyo.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo pamoja na kuwa umefikia hatua mzuri lakini changamoto ni kuwepo kwa miamba wakati wa uchimbaji wa mitaro ya utandazaji wa mabomba.

Amesema, watatekeleza maagizo ya Waziri Aweso ili kuhakikisha adhima ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo mama kichwani inafikiwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.