• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia awapongeza wafanyakazi, nao wamkubali

Imewekwa tarehe: May 1st, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mhe. Rais amesema hay oleo tarehe 01 Mei, 2021katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustion Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Athman Kattanga, Mawaziri, viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi ya Usalama na wafanyakazi wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzani (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.

Vilevile, Mhe. Rais amesema katika juhudi za kuboresha maslahi ya wafanyakazi Serikali ya Awamu ya Sita imeamua kupunguza kodi ya mishahara kutoka asilimia 9 ya mwaka 2020/21 hadi asilimia 8 kuanzia mwaka 2021/22, ameitaka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuharakisha mchakato wa kujadili, kufunga na kuidhinisha mikataba ya hali bora ya wafanyakazi, ameielekeza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwalipa mafao yao wastaafu ambao wamesubiri muda mrefu kuanzia mwezi huu na kulipa madeni ya watumishi.

Hatua nyingine ni kurejesha baadhi ya huduma za bima ya afya zilizokuwa zimeondolewa kufuatia marekebisho yaliyofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwaka 2018, kuongeza umri wa Watoto wategemezi wa bima ya afya kutoka miaka 18 hadi 21 na kuangalia uwezekano wa kugharamia matibabu kwa kundi la wastaafu bila kuzingatia kigezo cha miaka 10 ya uchangiaji, kuondoa tozo ya asilimia6 ya kulinda thamani ya mkopo kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Aidha, amesema Serikali inakusudia kuwapandisha vyeo watumishi 85,521 (ambao wataigharimu shilingi Bilioni449), kulipa malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya shilingi Bilioni 60, kufanya mabadiliko ya miundo ya utumishi yatakayogharimu shilingi Bilioni 120 na kuajiri watumishi wapya 40,000 ambao wataigharimu shilingi Bilioni 239.

Mhe. Rais Samia amesema kwa kutambua kuwa wafanyakazi wa sekta binafsi hawajapandishwa mishahara kwa miaka 8 na wafanyakazi wa sekta ya umma hawajapandishwa mishahara kwa miaka 6, amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama kufufua bodi za mishahara ili zifanyie kazi changamoto hiyo.

Kuhusu ombi la wafanyakazi kuongezewa mishahara, Mhe. Rais Samia amesema Serikali haitaweza kupandisha mishahara kwa sasa kutokana na changamoto za kushuka kwa ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 6.9 hadi 4.7 kulikosababishwa na janga la ugonjwa wa Korona na hatua za Serikali kuleta nafuu kwa wananchi kwa kurekebisha mfumo wa viwango vya kodi kunakotarajiwa kupunguza mapato.

Amewahakikishia wafanyakazi wote nchini kuwa miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa katika Awamu wa Tano chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli itaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa imo katika mpango wa Taifa wa maendeleo wa 3 wa mwaka 2021-26 ikiwemo miradi inayotekelezwa katika mkoa wa Mwanza ambayo ni ujenzi wa daraja ya Kigongo – Busisi, ujenzi na ukarabati wa meli katika Ziwa Victoria, ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Mwanza - Isaka.

Pia amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za elimu, maji na afya ikiwemo hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) hatua ambazo zitaendelea kulijenga Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamhokya amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuungana na wafanyakazi katika maadhimisho hayo na amemhakikishia kuwa wafanyakazi wote wanamuunga mkono na wapo tayari kutimiza wajibu wao kwa maslahi ya Taifa.

Mhe. Rais Samia amerejea Jijini Dodoma.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.