• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia aweka jiwe la msingi barabara ya pete

Imewekwa tarehe: February 10th, 2022

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3 huku akieleza namna anavyoisikia sauti ya mtangulizi wake hayati Dkt.John Magufuli akimtaka kuendeleza miradi mingine yote aliyoiacha .

Rais Samia amesema atahakikisha anaiendeleza miradi yote iliyoachwa na Hayati Dk. Magufuli na kuwataka wananchi kuitunza.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 9, 2022 wakati akizungumza katika ghafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa arabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la DODOMA( km 112.3).

Rais Samia amesema siku ya leo toka asubuhi anasikia sauti ya mtangulizi wake ikimueleza kuhusu miradi aiyoiacha ikiwemo ya kuhamia Dodoma
na mingine ikiwemo huu wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma.

“Ndugu zangu siku kama ya leo mimi mwenzenu toka asubuhi nasikia sauti ya mtangukizi wangu Dkt John Pombe Magufuli ananiambia kuhusu miradi hii ,,kuhusu dodoma kuwa makao makuu, kuhusu mambo mengi,

Na leo hii tupo hapa kuweka jiwe la msingi la mradi huu lakini kàzi hii waswahili wanasema ukiona vinaelea vimeundwa na kwa bahati nzuri muundaji wa suala hili aliyetekeleza maono ya taifa kuhamia Dodoma akataka kuipanga Dodoma ,kwa bahati mbaya hatunaye,Mungu amemchukua,

Lakini ameniachia urithi mzito nami niahidi mawazo yote aliyoyaanzisha nita kwenda kuyatekeleza kikamilifu,leo hii ni moja kati ya mawazo aliyoyaanzisha niahidi pamoja na kuungwa mkono na African Bank tunaenda kukamilisha mradi huu kama alivyotaka Magufuli,”alisisitiza Rais Samia.

Katika hatua nyingine Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1 ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.

“Ndugu zangu Benk kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benk kwa ajili ya waafrika,”amesema

Amesema kilomita moja ni shilingi bilioni 1.2 hadi 5 hivyo amesema Serikali inatumia fedha nyingi hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania Kutunza Miundombinu na kuacha mambo ya hovyo yanayofanywa Katika uharibifu huo.

Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga barabara 23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.

“Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya tano kuleta vuguvugu hili pamoja na kuungwa mkono na Benk ya Maendeleo na hawapo katika barabara wapo pia katika maji na umeme tumewaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu,”amesema

Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema lengo la kujenga barabara hiyo ni kupunguza msongamano katika Jiji la Dodoma.

Amesema jumla ya gharama ya Mradi huo ni shilingi bilioni 249 ambazo ni Kwa ajili ya fidia na ujenzi ambapo amedai kuna miradi midogo midogo kama ujenzi wa vituo vya afya,ununuzi wa ambulance wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Mtendaji huyo wa TANROADS ameeleza kuwa lengo ni kupunguza msongomana mkubwa wa magari katika Mkoa wa Dodoma ambao ungesababishwa na muingiliano wa magari yanayosafiri kupitia mjini.

Ameeleza kuwa barabara hiyo ina umbali wa Kil 20 kutoka katikati ya Jiji la dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni M/sAVIC INTL Project na China Civil Engineering Construction Cooperation zote kutoka Jamhuri ya watu wa China.

Alifafanua kuwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu na Nala.

Kwa upande wake,Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB) Dk.Akinwumi Adesina amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amedai wanaamini Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji.

Amesema Benki hiyo imewekeza kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 2.5.

“Miaka kadhaa iliyopita nilikaa na kuzungumza na rafiki yangu,mtu wa watu hayati Dk.Magufuli kuhusu kutekeleza mradi huu ,Kwa bahati mbaya hayupo tena lakini Kutokana na ushirikiano wake kwetu tunaahidi kuendelea kishirikina na watanzania kwa miradi mingi zaidi,”amesema.

Naye,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa Kujenga barabara hiyo kutokana na ongezeko la watu pamoja na Dodoma kuwa Makao Makuu hivyo magari yanayoingia na kutoka kuwa mengi.

“Tunatoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kutekeleza mradi huu,imetoa fedha nyingi katika miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya wakandarasi,

Bila kuwa na Mahusiano mazuri hili lisingetokea niipongeze Wizara kwa mradi huu mkubwa ni ubunifu mkubwa na utafungua fursa nyingi hivyo ” alisema.




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.