RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suhulu Hassan, leo tarehe 05 Desemba, 2021 amefungua rasmi Barabara ya New Bagamoyo sehemu ya Morocco hadi Mwenge yenye urefu wa Kilomita 4.3 kwa ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA.
Sherehe za ufunguzi wa barabara hizo zilizofanyika Kijitonyama ni sehemu wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru ambapo Mhe. Rais Samia anakagua, kuweka mawe ya msingi na kufungua baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji la Dar es Salaam.
Mhe. Rais Samia amesema ufunguzi wa barabara hiyo ni hududi za Serikali katika kuboresha na kujenga miundombinu ya barabara katika Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kupnguza kero ya msongamano wa magarai na ajali za barabarani katika Jiji hilo.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka wananchi kuzingatia sheria ili kupata manufaa yaliyokusudiwa katika kujenga barabara na miundombinu kwa kuepuka kufanya vitendo vitakavyopelekea uharibifu wa miundombinu hiyo.
Pia, Mhe. Rais ameitaka Wizara ya Ujenzina Uchukuzi pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa barabara na madarajaunafanyika kwa viwango vilivyokubaliwa kimkataba ili zidumukwa muda uliokusudiwa.
Kuhusu Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Rais Samia amesemakuwa sura ya Jiji imebadilika kwa kiasi kikubwandani ya miaka mitano iliyopita hasa katika miundombinu ya barabara kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kuwezesha mitaa mingi kuwa na barabara za lami huku akitole mfano Magomeni na Kinondoni.
Mhe. Rais Samia amesema Serikali inaendeleana kuboresha miundombinu mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kwa sasa inaangalia uwezekano wa kuboresha eneo la Jangwani ambalo limekuwa kero kwa wananchi hususani kipindi cha mvua.
Vilevile, Mhe. Rais Samia amewakumbusha wananchi kuendelea kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 kutokana na tishio la wimbi la nne la ugonjwa huo ambalo limezikumba nchi mbalimbali duniani.
Kuhusu fedha za mkopo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Mhe. Rais Samia amesema matumizi ya fedha hizo hayahitaji ufuatiliaji makini na kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Serikali imeanzisha kitengo cha tathmini na ufatiliaji ili kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amewatembelea mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyererena mjane wa Hayati Rais Benjamin Mkapa Mama Anna Mkapa, kuwasalimia na kuwajulia hali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.