RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 16 Oktoba, 2022 ameanza ziara ya kikazi Mkoani Kigoma ambapo amezindua rasmi hospitali mpya ya wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma ambayo imeanza kutoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo ya jirani.
Ujenzi wa hospitali hiyo imegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.5 ikijumuisha gharama za ujenzi wa majengo, vifaa tiba na fidia kwa wananchi.
Rais Samia amesema hospitali hiyo itasaidia wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya ambazo zilikuwa zikipatikana Kibondo, Kahama na Runzewe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.