• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia azindua Kiwanda cha kutengeneza Nyaya za Mawasiliano

Imewekwa tarehe: December 3rd, 2021

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 03 Desemba, 2021 amezindua Kiwanda cha Kutengeneza Nyaya za Mawasiliano cha Raddy Fiber Manufacturing Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho, Mhe. Rais Samia amesema hafla hiyo ni sehemu ya Maandhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo ameanza kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mheshimiwa Rais Samia amesema uzinduzi wa kiwanda hicho unathibitisha uwezo na fursa nyingi ambazo nchi yetu imejaliwa kuwa nazo na ziweze kutumika ili kukuza uchumi wa nchi, kuleta ajira kwa wananchi hususani vijana na kuzalisha bidhaa ambazo sio lazima kuagizwa kutoka nje.

Aidha, Mhe. Rais amemshukuru na kumpongeza mwekezaji wa kiwanda hicho Bw. Ramadhani Hassani Mlanzi ambaye ni mzawa kwa kuona kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na kumhakikishia kuwa Serikali itampa ushirikiano wa kutosha.

Vilevile, Mhe. Rais Samia amewakaribisha wawekezaji wengine kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza Tanzania na kuwahakikishia usalama wa mitaji yao pamija na uhakika wa kutengeneza faida.

Pia, Mhe. Rais Samia amesema Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi nchini katika kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi hivyo inaendelea kiweka mazingira wezeshi na rafiki ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

Mhe. Rais ameagiza taasisi zote za Serikali zinazotoa huduma katika sekta ya uwekezaji kuondoa urasimu ambao umesababisha kupoteza baadhi ya wawekezaji waliokuwa wanataka kuwekeza nchini kwa kuwa wawekezaji wana mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi yetu.

Vilevile, Mhe. Rais Samia amesema Serikali itaimarisha jitihada za mageuzi ya kisera na kisheria ikiwemo utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini ujulikanao kama The Blueprint for Regulatory Reforms to Improve Business Environment.

Mhe. Rais Samia ameongeza kuwa Serikali ina lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma za mawasiliano ili kuwezesha kutumia huduma zitokanazo na TEHAMA katika kukuza uchumi nchini.

Aidha, Mhe. Rais Samia amemtaka Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd kuwa anakamilisha azma yake ya kujenga kiwanda cha kuzalisha simu janja (smart phone) hapa nchini ambacho pia kitachangia utoaji wa ajira kwa vijana. 

Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd kina uwezo wa kuzalisha kiasi cha kilomita 24,000 za optic fiber kwa mwaka na kinatarajiwa kutoa ajira zipatazo 670 kitakapokamilika katika awamu zote na hivyo kukifanya kuwa kiwanda cha tatu kwa ukubwa barani Afrika na cha kwanza kwa Afrika Mashariki na Kati.

Awali akiwa njiani kuelekea Mkuranga, Mhe. Rais Samia alipata fursa ya kuwasalimia wananchi wa Mbagala Zakhem na Vikindu mkoani Pwani ambapo amewahakikishia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga kuwa kwa sasa Serikali inajenga mazingira bora zaidi ambayo yatawawezesha kufanya biashara kwa uhuru na katika msimu wote wa mwaka.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.