RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Juni 2021 amezindua mitambo ya kisasa ya uchunguzi na matibabu ya moyo Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo, mitambo yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.6 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais amesema mitambo hiyo ambayo ina uwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ni wa kwanza hapa nchini na wa pili Afrika Mashariki na hivyo imesaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo ya moyo nje ya nchi kwa kuwa sasa wanatibiwa hapa nchini.
Aidha, Mhe. Rais ameisifu Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kuokoa maisha ya wananchi wenye matatizo ya magonjwa yasiyo ambukiza ikiwa ni Pamoja na moyo kwa kutumia wataalam wake wa ndani ambao wengi wao ni vijana na kuahidi kuboresha maslahi yao.
Vile vile, Mhe. Rais amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima kushughulikia ombi la Taasisi Moyo Jakaya Kikwete la kurejeshewa asilimia 30 ya fedha ambazo husamehewa baadhi ya wagonjwa ili ziweze kuendeleza huduma hospitalini hapo.
Mhe. Rais Samia amesema amefarijika na taarifa kuwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hutibu wagonjwa wa mataifa mbalimbali kama vile Comoro, Burundi, Ethiopia, Malawi na Marekani na hivyo kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utaoji huduma za Kibingwa bobezi barani Afrika.
Amesema hivi sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya upanuzi wa miradi 22 ya hospitali za rufaa, mikoa, kanda na hospitali maalum kwa gharama ya shilingi Bilioni 193 ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha huu Serikali imepanga kuendeleza hospitali za wilaya 99 na kuanza ujenzi wa hospitali mpya za wilaya 28 na kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya 52 na vituo vipya 121 na kumalizia maboma ya zahanati 763 yenye gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 198.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima ameishukuru Serikali kwa kutoa ajira zaidi ya 3,000 kwa sekta ya afya ikiwa ni jitihada za kuimarisha afya za Watanzania.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi amesema Serikali imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 250 ambazo awali zilikuwa zikitumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi na kuokoa Maisha ya Watanzania 444,848.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI mara alipotembelea chumba cha Wodi ya Watoto wenye uhitaji wa Uangalizi maalum kabla ya kuzindua mitambo ya Catheterization Laboratory pamoja na Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system katika Taasisi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi alipokuwa akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa mitambo hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi wakati akitoka kutembelea Wodi ya Watoto katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo pamoja na kukagua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.