RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Kigoma kuilinda na kuitunza miundombinu ya umeme iliopita mkoani humo ili iweze kuwaletea manufaa katika shughuli zao za maendeleo.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua umeme wa gridi ya taifa na kuzima umeme wa jenereta kutoka megawatt 14 hadi megawatt 20 wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Aidha, Rais Samia amesema kwa hivi sasa mkoa wa Kigoma utapata umeme wa moja kwa moja na wa uhakikka ambao utavutia wawekezaji mkoani humo na hivyo kukuza uchumi.
Rais Samia ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma ambapo leo amezindua majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Kabanga wilayani Kasulu ambayo yamejengwa na Serikali chini ya Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ualimu Tanzania (TESP).
Vile vile, Rais Samia amezindua na kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa barabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo - Kibingo/Kakonko, kufungua barabara ya Kadhwe - Kasulu pamoja na kufungua Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.