Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka leo tarehe 10 Novemba, 2021 kuelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
Ziara hiyo ya Kiserikali ya siku tatu inafuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi, imesema taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka kwa Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia Pamoja na mambo mengine anatarajia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.
Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji Saini mkataba mmoja (1) na hati saba (7) za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kabla ya kuondoka nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Chanzo: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.