RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amewasiri jijini Dodoma tayari kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho.
Rais Mwinyi amewasiri Jijini Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge katika uwanja wa ndege jijini hapa.
Uzinduzi rasmi wa Bunge la 12 la Muungano utafanyika kesho ambapo Mhe. Rais Dkt. John Magufuli atalihutubia Bunge hilo baada ya leo kuwasilisha jina la Waziri Mkuu mteule Kassim Majaliwa ambaye wabunge wote 350 waliokuwepo walimpigia kura ya ndiyo kuthibitisha uteuzi unaomfanya kuendelea kushikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha pili cha Serikali ya awamu ya tano.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.