Na. Coletha Charles, DODOMA
Mtaa wa mkonongo kata ya kizota wametangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo chama cha mapinduzi (CCM) Kimeibuka kidede kwa ushindi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wake watano.
Matokeo hayo yametangazwa tarehe 27 novemba na mtendaji wa mtaa wa mkonongo, Lizboter Edward, katika ofisi ya kata kizota low cost amesema kuwa uchaguzi ulikuwa wa amani bila ya vurugu zozote.
“Matokeo ya mwenyekiti idadi ya waliojiandikisha kupiga kura 2,203, idadi ya walipopiga kura 1,943, idadi ya kura halali 1,940 na idadi ya kura zilizoharibika ni 3 kwahiyo Ramadhan Msalange Kambega CCM amepata kura 1,850 na Shaban Juma Makufuri wa ACT WAZALENDO amepata kura 93 kwa mamlaka niyopewa namtangaza Ramadhan Kambega kuwa mwenyekiti wa mtaa’’.
“Wajumbe mchanganyiko na kundi la wanawake idadi ya waliojiandikisha kupiga kura 2,203, idadi ya waliopiga kura 1,943, idadi ya kura halali 1,940 na idadi ya kula zilizoharibika ni 46 ambapo Chama Luchanganya CCM amepata kura 1,777, Rehema Elias CCM kura 1,777, Mwanahamisi Ramadhani CCM kura 1,777, Shamira Ally CCM 1,700, Edina Mwanjila CCM kura 1,695 na Athanasio Makole ACT WAZALENDO amepata kura 139.” alisema Edward.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.