Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Maduka Paul Kessy ameiomba serikali kulisaidia Jiji la Dodoma kupata mikopo na pia kulisaidia kutimiza jukumu la kuongoza ujenzi wa Makao Mkuu ya Serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb). Kessy alikuwa akitoa salamu zake kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aweze kumkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa TAMISEMI kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo mawili ya vitegauchumi vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyofanyika tarehe 27/08/2019 kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
"Ombi waliloliweka mezani kwako ya kwamba Jiji la Dodoma linatakiwa katika misingi yoyote ile liangaliwe katika hali ya mkakati wake. Ni vema likaangaliwa kupata mikopo ambayo itaweza kuharakisha maendeleo ya Mji Mkuu wa Serikali" alisema kwa msisitizo Kessy.
Aidha, Katibu Tawala Kessy alifafanua kuwa Jiji la Dodoma linatakiwa kupima viwanja, kuweka miundombinu na kuwezesha mambo mengine mbalimbali kwa lengo la kujenga mji mkuu wa kisasa wa karne ya 21.
Hivyo basi, alisema Jiji la Dodoma linatakiwa liangaliwe...liweze kubeba uwezo wake wa kuongoza ujenzi wa Makao Makuu ya Serikali nchini.
"Kama haya hayatafanyika, basi ni vigumu sana tukaenda na kasi tunayoitarajia kwenda nayo katika ujenzi wa Makao Makuu ya nchi" alisisitiza Katibu Tawala huyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.