Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amempendekeza Mbunge wa Ruangwa Mhe. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kipindi cha pili cha Serikali ya awamu ya tano mbele ya Bunge.
Wabunge wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakapata nafasi ya kupiga kura kuthibitisha uteuzi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.
Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na Wabunge, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Majaliwa amepigiwa kura 350 na hakuna kura iliyoharibika hivyo amepitishwa kwa asimilia 100%.
Akiongea kwa unyenyekevu, Mhe. Kassim Majaliwa alimesema “Jambo hili si dogo, namshukuru sana (Dkt. Magufuli) kwa imani yake kubwa aliyonayo juu yangu na kuendelea kuniamini kwamba naweza kufanya niliyofanya katika kipindi cha miaka mitano na zaidi katika kipindi kingine kijacho,
Niendelee kumhakikishia kwamba matamanio yake yaliyompelekea kutoa jina hilo kulileta mbele ya bunge hili tukufu ambayo anaamini na wabunge wenzangu kwa namna ambavyo mmepiga kura nyingine ni namna tosha mheshimiwa rais ameleta jina ambalo mnaamini nitamsaidia kazi, nami niwahakikishie nitafanya hivyo” amesema Majaliwa kwa kujiamini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.