• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rasmi, Ujenzi wa mahandaki reli ya kisasa - SGR Morogoro - Dodoma wazinduliwa Kilosa

Imewekwa tarehe: July 23rd, 2019

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Atashasta Nditiye amezindua rasmi uchorongaji milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki (tunnels) yatakayopitisha reli ya Kisasa – Standard Gaude Railway (SGR) kipande cha Morogoro – Makutupora Dodoma katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro  hivi karibuni .

Jumla ya Mahandaki 4 yenye jumla ya urefu wa Kilometa 2.6 yanatarajiwa kujengwa katika Mradi wa SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa ambapo handaki refu zaidi nchini linatarajiwa kujengwa likiwa na urefu wa Kilometa 1.031 sambamba na mahandaki mengine matatu ambayo yote kwa pamoja yataunganishwa na madaraja makubwa ili kuepusha athari za mafuriko ya mto mkondoa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mbunge wa Kilosa, Menejimenti na Wafanyakazi wa TRC na Yapi Merkezi, wanahabari pamoja na wananchi wa wilaya ya Kikosa katika Milima ya Kilosa mkoani Morogoro.

Waziri Nditiye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kwa Usimamizi mzuri wa Miradi na kuwataka waendelee kuchapa kazi ili kuleta tija na matokeo mazuri katika utoaji huduma bora za usafiri wa reli.

Aidha Naibu Waziri amewashukuru wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano wanaoonesha kwa wakandarasi na TRC, pia amewatoa hofu wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kuwa endapo serikali itahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi, mwenye eneo atalipwa fidia pamoja na stahiki nyingine anazostahili kulipwa.

“Napenda niwahakikishie watanzania, kwa yule ambaye tutamfuata kwenye eneo lake tutamlipa fidia yake” Amesema Mhe. Atashasta

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa ameongeza kuwa uthaminishaji wa ardhi ili kukabidhi maeneo yaliyobaki kwa mkandarasi unaendelea na majedwali ya fidia yanafanyiwa kazi.

Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Atashasta Nditiye akikata utepe jana Julai 22, 2019 kuashiria kuanza rasmi kazi ya uchorongaji  milima kwa mara ya kwanza Shirika la Reli Tanzania kwa ajili ya mahandaki ambayo watatumia kupitisha reli ya kisasa-SGR kwa kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa Morogoro- Makutupora Dodoma tukio hili lilifanyika katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Atashasta Nditiye akipewa maelezo baada ya kukata utepe.


Muonekano rasmi wa uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki (tunnels) yatakayopitisha reli ya Kisasa – SGR kwenye kipande cha Morogoro hadi Makutupora Dodoma, tukio hili lilifanyika katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro hapo jana.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.