Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewahimiza wananchi wa Dodoma kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF iliyoboreshwa) ili iwasaidie kupata huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu.
Dkt. Mahenge aliyasema hayo wiki iliyopita (14 Mei, 2020) alipokuwa akizindua kampeni ya uhamasishaji wananchi wa mkoa wa Dodoma, kampeni itakayotumia njia mbalimbali kuwafikia wananchi ikiwemo kupitia vyombo vya habari.
CHF iliyoboreshwa kwa sasa inatekelezwa nchi nzima na hivyo wananchi wanachangia kiwango kimoja ambacho ni shilingi 30,000/= (elfu thelathini) tu kwa kaya yenye watu 6 kwa mwaka mzima. Hii ni sawa na kila mtu kuchangia shilingi 5,000/= kwa mwaka.
Alielezea zaidi Dkt. Mahenge ametanabaisha kuwa taarifa ya maendeleo ya Mfuko wa CHF kwa kipindi kilichoishia Juni, 2019 mkoa wa Dodoma ulisajili jumla ya kaya 17,366. Kuanzia mwezi wa Julai, 2019 hadi Aprili ,2020 hali ipo kama ifuatavyo:
Akimalizia Mkuu wa Mkoa alisema kuwa "ni imani yangu tukifanya kazi kwa ushirikiano katika kutekeleza mikakati hii tuliyojiwekea na maelekezo haya tuliyopeana katika kazi hii, tukiweza kufika vijijini/mitaa yote katika Mkoa wa Dodoma tutasajili kaya zote ambazo hazina kadi za CHF". Dkt. Mahenge alimalizia maelezo yake kwa kuzindua rasmi kampeni ya uhamasishaji jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF iliyoboreshwa) kwa mwaka 2020.
Bofya hapa kusoma hotuba ya uzinduzi: HOTUBA YA UZINDUZI WA UHAMASISHAJI CHF 2020 RC DODOMA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.