MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amemuagiza Mhandisi wa Maji (RUWASA) Wilaya ya Mpwapwa katika eneo la Mtera kukarabati kwa wakati miundombinu ya upelekaji maji kutoka katika bwawa la Mtera kwenda kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya jirani.
Dkt. Mahenge alisema hayo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua ukarabati miundombinu ya maji ambayo inatoka katika bwawa la Mtera na kwenda kwa wananchi.
Aidha, Mahenge amesisitiza kuwa wananchi wanauhitaji mkubwa wa maji na Mheshimiwa Rais ameshatoa maagizo tangu awali wananchi waweze kupata huduma ya maji katika bwawa hilo lakini pia matarijio ya mji kuwa mkubwa hapo baadae ni makubwa mno katika eneo hilo la Mtera.
"Nimembelea na kukagua miundombinu yote, ninachokiona kinaweza kurahisisha sisi kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais, wananchi kupata maji kwa uhakika kutoka katika bwawa hili la Mtera. Kwa maana hiyo kwa awamu hii ya kwanza mnahitajika kurekebisha mashine hizi za mwanzo mbili na kuongeza ukubwa wa kipenyo cha bomba kinacho toa maji kwa wananchi wakati tukiendelea kusanifu mradi wa muda mrefu kwani tuna matajarajio ya mji huu kuja kuwa mkubwa na mahitaji ya maji yataongezeka” alisema Dkt. Mahenge.
Vile vile, kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa wamepokea maelekezo yote kutoka kwa mkuu huyo na watayatekeleza kama alivyokwisha kuelekeza hapo awali wakiwa wanafanya ukaguzi katika miundombinu hio. "Tunakushukuru Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwa ziara yako ya ukaguzi wa utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais kuwa wananchi wa maeneo haya ya Mtera waweze kupata maji. Maelekezo yako tumeyachukua na tutayafanyia kazi ipasavyo ilituweze kufanikisha mradi huu kwa awamu ya kwanza huku tukiendelea kusanifu mradi mkubwa na wa muda mrefu kutokana na matarajio yetu ya eneo hili la Mtera kuwa na ongezeko la uhitaji wa maji’’ alisema Mhe. Shekimweri.
Hata hivyo, Mhandisi wa Maji (RUWASA) Mkoa wa Dodoma, Godfrey Mbabaye ametoa tathmini ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa utakaokidhi ongezeko la mahitaji ya watu ambapo mradi huo utaghalimu shilingi Bilioni 1.6 na kwa hatua za awali wameishaanza usanifu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa agizo la Rais kuhusu maji kuwafikia wananchi wa jirani na Bwawa la Mtera.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.