Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amefanya ziara kwenye kata za Ihumwa na Chahwa jijini Dodoma ili kusikiliza kero za wananchi katika kata hizo.
Akiwa kwenye kata ya Ihumwa mkuu wa mkoa alisikiliza kero za wananchi wa eneo hilo huku kero kubwa ikiwa ni ukosefu wa maji
Mahenge pia alitembelea kata ya Chahwa ambapo kero kubwa katika eneo hilo ilikua ni migogoro ya ardhi, umeme pamoja na maji. Wakizungumzia ardhi, baadhi ya wanachi waliopimiwa maeneo yao ili kupicha ujenzi wa Ikulu takribani kaya 18 hawajalipwa fidia zao na kaya mbili bado wanaishi ndani ya eneo hilo.
Akijibu kero hiyo Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma Helman Tanguye amesema taarifa hizo wanazo na hali hiyo imetokana na wananchi hao kutoridhika na tathimini iliyofanywa na Wakala wa Majengo hivyo maeneo yao yamepimwa tena na zoezi hilo limekamilika na taarifa hiyo ipo makao makuu tayari kwa ajili ya zoezi la kuwalipa wananchi hao.
Katika ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa aliambata na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ambaye alijibu hoja ya sintofahamu kuhusu uwanja wa mpira pamoja na ofisi ya kata vilivyojumuishwa katika eneo la Ikulu bila fidia yoyote.
Akijibu hoja hiyo Kunambi alisema, maeneo hayo yote ni mali ya halmashauri ya jiji, hivyo hayapaswi kulipiwa fidia, isipokua wao kama jiji watatenga maeneo kwa ajili ya kiwanja hicho na ofisi ya kata.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi amesisitiza kuwa maeneo ya wazi ni maeneo ya umma hivyo maeneo hayo ni mali ya wananchi na yatatumika kwa faida ya watu wengi zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.
Nae Kaimu Meneja wa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mhandisi Wolta Kirita amesema kuwa Kata ya Chahwa imeingizwa katika mpango wa Mwezi Novemba na eneo hilo limeshasanifiwa tayari kwaajili ya kujenga mradio huo.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Wa Tanesco mkoa wa Dodoma Lupenza amesema wapo kwenye hatua nzuri kuhakikisha umeme unafika katika kata hiyo na tayari wamesha sambaza nguzo za umeme na kuwaahidi kuwa mpaka ifikapo mwezi Disemba umeme utakuwa umefika katika maeneo yao.
Akifunga mkutano huo Mkuu wa Mkoa amewapongeza Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde, Diwani wa Kata ya Chahwa na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza na kutoa kero zao na kuwaahidi kuwa atazifanyia kazi na kuzimaliza kero zao.
"Jiji litaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya huduma za jamaii" amesema Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma (aliyeshika kipaza sauti) alipokuwa akijibu baadhi ya kero za wananchi wa Ihumwa jijini Dodoma leo.
"Maeneo ya wazi ni mali ya umma,... yatatumika kwa faida ya watu wengi zaidi" - Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi amesema wakati za ziara ya Mkuu wa Mkoa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.