Na Nemes Michael, DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amefanya mkutano wa wazi na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, nyumbani kwake Kata ya Zuzu jijini hapa, ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, mazingira na taasisi za kifedha, ukiwa na lengo la kuimarisha kilimo, viwanda, elimu, na uhifadhi wa mazingira.
Mkuu wa Mkoa Mtaka alisema kuwa, sekta ya mazingira na kilimo ni kipaumbele katika mikakati ya mkoa wa Dodoma ambapo anatazamia kuimarisha sekta hizo kwa mazao yanayopatikana jijini hapa, vilevile kuhakikisha upandaji miti katika kuimarisha mazingira na kupambana na athari zake.
“Katika utekelezaji tutahakikisha tunapata wakati sahihi kuzungumza na wadau wa kilimo na wafanyabiashara wa zao la zabibu katika kujadili namna bora ya kuinua zao zabibu pamoja na mazao mengine, naamini kupitia hatua hiyo tutapata mawazo sahihi katika kufikia malengo na kuonyesha utofauti” alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alisema kuwa zabibu ni zao mama kwa Mkoa wa Dodoma na linahitaji kipaumbele na mikakati maalum katika kuhakikisha faida inaonekana na kupatikana kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo.
“Tunahitaji kutambua kuwa zabibu ni zao la kudumu la biashara kwenye Mkoa huu, lakini lazima ushawishi uwepo katika utoaji kipaumbele kwenye zao hili na kuonyesha utofauti na mazao mengine na kuipa heshima Dodoma kupitia zao hili” alisema Mhe. Pinda.
Naye, Mkugenzi Mtendaji benki ya Maendeleo ya Kilimo Japhet Justine alisema kuwa utayari katika utendaji ni kitu cha kuzingatia, na kwamba anaahidi ushirikiano chanya kutoka katika benki hiyo kama mdau mkubwa wa sekta ya kilimo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.