Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo inayoendelea na kutakiwa kufikiria kuanzisha miradi mingine katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kusogeza huduma kwa wananchi na kuongeza mapato yake.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini hapa leo tarehe 20 Oktoba 2021.
Mhe. Mtaka alisema “Halmashauri ya Jiji la Dodoma ijipange kuanzisha miradi mikubwa mingine katika kipindi cha miaka mitano. Miaka mitano iliyopita, Halmashauri ya Jiji imeanzisha na utekeleza miradi mingi mikubwa na mizuri, hongereni sana”.
Aidha, aliitaka halmashauri hiyo kufanya kazi kwa upekee ikilinganishwa na maeneo mengine nchini. “Halmashauri ya Jiji la Dodoma mna madiwani bora sana kwa sababu mmekaa pamoja na kuelewana. Umoja huo uwasaidie viongozi wa Halmashauri ya Jiji kutatua migogoro na kutekeleza miradi ya maendeleo. Wekeni mkakati wa kupata mawazo ya watumishi wa ngazi za chini kwa sababu wana mawazo mazuri ya kuisaidia halmashauri” alisema Mhe. Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepanga kifanya vikao na halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kuongea na watumishi ili kuweka dira ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mkoa huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.