MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa kata wa Chihanga kutoa ushirikiano kwa Serikali popote wanapohitajika kwani hakuna Serikali yenye dhamira mbaya kwa watu wake ili katika kutatua changamoto za uvamizi katika chanzo cha maji cha Bonde la Mzakwe.
Senyamule ameyasema hayo juzi Septemba 27, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Chihanga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Amesema lengo la ziara yake katika Kata hiyo ni kuendelea kutekeleza maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuongea na wananchi, kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi.
"Ndugu zangu naombeni mtoe ushirikiano hakuna Serikali yenye dhamira mbaya na wananchi wake na mnamfahamu Rais wenu hataki kusikia mtu ananyanyaswa wala kupigwa, anataka wananchi wake wawe na amani na wasikilizwe kero zao ili kuendelea kudumisha umoja na mshikamano wa Tanzania."amehimiza Senyamule
Pia, Mkuu huyo wa Mkoa amekemea suala la utoro wa watoto na kuwaagiza wazazi ambao watoto wao wamefaulu na kubaki nyumbani bila sababu za msingizi amewahakikishia hatua za kisheria zitachukulia kwani ni kinyume na taratibu za nchi kwakuwa kila mtoto anatakiwa kupatiwa haki yake ya kupata elimu na tayari kuna miundombinu wezeshi hivyo wanatiwa kuzitendea haki.
Naye, Afisa Mazingira Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Bw. Rajabu Mwinyialipo amesema elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wanaoishi jirani na ndani ya Bonde hilo kuhusu namna ya kuendelea kukilinda chanzo hicho cha maji ya Bonde la Mzakwe kwani ndio tegemeo ndani ya Jiji la Dodoma kwa kukizingatia kwa sasa ni Makao Makuu ya nchi.
Vile vile, Bw. Mwinyialipo ametaja baadhi ya shughuli za kibinadamu ambazo hazitakiwi kufanyika ndani ya Bonde hilo kuwa ni pamoja na Kilimo, uchomaji wa mkaa, uchimbaji wa visima na ufugaji kwani zitasababisha uharibifu wa Bonde na kupelekea changamoto ya maji ndani ya jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.