MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amekagua ujenzi wa uwanja mpya wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma.
Senyamule alipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo kutoka kwa Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali bwana Meshach Bandawe. Bandawe alisema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huo unahusisha eneo la uwanja wa gwaride na Mnara wa Mashujaa ambao unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Juni 2023.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe ambaye pia anakaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, pia aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma, viongozi wa taasisi za Serikali na watendaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule (wa nne kutka kushoto) alipotembelea eneo linalojengwa Uwanja mpya wa Mashujaa kwenye Mji wa Serikali Jijini Dodoma akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe ambaye pia anakaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma (wa kwanza kushoto) na maafisa wengine wa Serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.