MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua Kliniki ya Matibabu ya Kibingwa yanayotolewa na Madktari
walio chini ya Kanisa la Seventh day Adventist Movement (Wasabato) katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo inayotolewa bila malipo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma umeungana na Mataifa mbali mbali kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani.
“Huduma hizi zimeanza tangu tarehe 15 Julai na zitahitimishwa tarehe 25 Julai 2024 ambapo magonjwa mbali mbali yanapatiwa matibabu ikiwemo magonjwa ya Kibingwa kama vile Moyo, Meno, macho na magonjwa mengine.
“Ni fursa kubwa ambayo tumeipata Katika Mkoa wetu. Muhimu ni kwamba kuja hapa kwa wananchi wa Dodoma ni bahati kupata huduma za namna hii ambazo zinatolewa bila malipo kuanzia kumuona Daktari, matibabu hadi Dawa Si jambo la kawaida sana lakini wenzetu wamekuja wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kuwafikishia huduma iliyo bora” Mhe .Senyamule
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Thomas Rutachunzibwa amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Kanisa hilo imefanikisha kuweka kambi maalumu kwa ajili ya huduma za kibingwa na kufanikisha taaluma zote za afya na kuna Madaktari kutoka ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni wananchi wafurahie huduma hizi zinazotolewa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.