Na. Arafa Waziri, MNADANI
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule azindua Maktaba mpya katika Shule ya Sekondari Mnadani iliyopo Kata ya Nkuhungu jijini Dodoma.
Maabara hiyo imekarabatiwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 20 kwa msaada wa Taasisi ya Genesis kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA
Akizungumza baada ya uzinduzi huo Senyamule aliishukuru Taasisi ya Genesis kwa Mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa kwenye sekta ya elimu nchini.
‘’Niwashukuru sana na kuwapongeza Taasisi ya Genesis kwa kazi kubwa mnayoifanya kwa kujali na kusaidia serikali katika jitihada za kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri kwa kurekebisha Maktaba shuleni. Maktaba hii itaongeza chachu ya usomaji kwa wanafunzi hivyo, kiwango cha taaluma kitaongezeka ‘’ alisema Senyamule
Aidha, Senyamule pia aliwaasa wanafunzi hao kutumia vizuri Maktaba hiyo kwa kusoma kwa bidii na kuongeza Maarifa ili waweze kuongeza kiwango cha taaluma shuleni hapo. ‘’Tukitumia vizuri Maktaba hii tutakuwa na ujuzi na maarifa. Lengo la Genesis kuboresha maabara hii kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujisomea pia kuhakikisha ufaulu unaongezeka hivyo, tunategemea mtaitumia vizuri maktaba hii katika kuleta matokeo chanya kwenye elimu” aliwaasa.
Aidha Senyamule alipongeza walimu kwa kazi nzuri wanazoendelea kuzifanya na alitoa wito kwa Walimu shuleni hapo kusimamia vizuri Matumizi mazuri ya Mktaba hiyo kwa wanafunzi. ‘’Mkiwahamasisha wanafunzi matumizi ya Maktaba maana yake kazi pia itakuwa rahisi kwenu walimu hivyo, ni wajibu wenu kama walimu kuwafundisha matumizi mazuri ya Maktaba ili kazi nzuri ya Genesis iweze kuzaa matunda’’ Alisema Senyamule.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Denis Mwamfupe alisema kuwa msaada wa Genesis ukawe mwanzo mzuri katika shule ya Mnadani na ukalete mapinduzi ya taaluma shuleni hapo. “Tunategemea kuona mabadiliko katika shule hii kitaaluma kupitia maktaba hii. Nawashukuru sana Genesis kwakuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha inaboresha miundombinu ya kujifunzia, niwaombe wanafunzi mkafate maelekezo ya walimu wenu na hakikisheni mnatumia maktaba hii kupata msaada katika masomo yenu ili mkawe wanafunzi bora’’ alisema Mwamfupe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.