Na. John Masanja
VIKUNDI vya 'Jogging Clubs' Mkoa wa Dodoma vimepongezwa kwa kuendelea kuwa na mshikamano na kuwa vinara wa kuhamasisha watu kufanya mazoezi kwa kuboresha afya zao na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kuelimisha jamii kupitia kampeni mbalimbali.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule baada ya kumalizika kwa mazoezi na mbio fupi zilizofanyika kwa kuratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na “Friends of Mavunde” na “Dodoma City Legends Family”.
“Katika makundi tuliyonayo kwa mkoa wetu hivi vilabu vya Jogging wamekuwa kinara wa kuimarisha mshikamano wao wenyewe na wafuasi sisi tunaoungana nao kufanya mazoezi, ni makundi ambayo hayana uvivu wa kufuatilia jambo lao wakiamua nawapongeza sana.
" Kupitia mchango wao wa kuhamasisha unatupa sisi fursa ya kufikisha ujumbee mbalimbali. Kwa jamii, jambo kubwa nimefurahi leo kwa sababu mazoezi haya ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wetu ya kila jumamosi ya pili ya mwezi iwe ni siku ya mazoezi kwaajili ya kutunza afya zetu na kupunguza magonjwa yasiyoambukiza. Leo ni Jumamosi ya pili ya mwezi Desemba kwaiyo, sisi tumetimiza maelekezo ya Rais wetu, hongereni sana", alisisitiza Senyamule.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Gwamaka Mlagila alisema “michezo ni afya na kutoa damu ni upendo na hakuna michezo bila upendo. Kwahiyo, niwahamasishe mjitokeze kwa wingi kuchangia damu ili ziwasaidie wagonjwa wanaohitaji damu”.
Vikundi vya "Dodoma City Legends Family na kikundi Cha Friends of Mavunde’' wametumia siku hii kufanya uzinduzi rasmi wa vikundi vyao na watashiriki mambo mbalimbali ya kurudisha furaha kwa jamii kwa kuwatembelea watoto yatima na kuchangia damu zitakazookoa maisha ya wengine. “Vikundi hivyo, vinafanya matendo hayo ya huruma kupitia kaulimbiu "Rejesha Tabasamu Kwao".
Akiwasikisha salamu za Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo na kuwataka wananchi waendelee kudumisha mazoezi ya mara kwa mara kwa ustawi wa afya za kula mmoja.
Zoezi la Jogging limeanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hadi katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma likikamilisha idadi ya kilometa 5 Kwa wakiambiaji na washiriki.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.