Na; Siza Kangalawe
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Dodoma kuanzisha kamati za ulinzi ngazi ya kata na mitaa ili kubaini watoto wanaotumikishwa na wazazi kama kitega uchumi.
Agizo hilo limetolewa wakati wa kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Jijini hapo.
“ Naziagiza Halmashauri zote kuanzisha kamati za ulinzi na usalama za Kata na Mitaa ili kubaini watoto wanaotumikishwa na wazazi kama kitega uchumi", Ameagiza Mhe. Senyamule
Sambamba na hilo Mhe. Senyamule amehimiza kila Halmashauri kuweka sheria ndogondogo zitakazo saidia kutoa adhabu kwa wazazi/walezi wanaowatumikisha watoto kwenye kazi za mtaani.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo ameainisha sababu zinazochangia uwepo wa watoto wa mtaani na ombaomba katika Mkoa huu zikiwemo hali ya kukua kwa Mkoa na Miji , kuwepo kwa migogoro katika ndoa, hali ya uyatima, ukatili ndani ya familia , umasikini na kukosekana kwa sheria ndogo ndogo katika Halmashauri zinazowajibisha jamii, wazazi na walezi wasiozingatia usimamizi wa haki za watoto na watu wenye ulemavu wanaotumikishwa.
Kwa upande wake Mfanyakazi kutoka Shirika la SOS Children’s Villages Bw. Damas Damas Amedeus amesema mbali na changamoto hizo wamekuwa wadau muhimu wa masuala ya watoto katika kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wanatimiza haki zao za msingi na kukabiliana na kadhia wanazozipata.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.