WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umejitayaridha kutenga Shilingi bilioni 6.7 kwa ajili ya kutengeneza mifumo ya utumiaji wa gesi asilia kwenye baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani na Lindi katika mwaka wa fedha 2023/24,
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Hassan Saidy ameyasema hayo jana katika mji wa Ifakara uliopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo na mwelekeo wa taasisi kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Mhandisi Saidy amesema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2023/24, REA itagawa rasilimali fedha zake kwenye sehemu mbili zikiwemo za kusambaza umeme vijijini na kusaidia upatikanaji wa nishati bora ya kupikia kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali inafanya kazi na taasisi binafsi na za umma kuhakikisha wananchi wanatumia nishati bora ya kupikia, sisi REA tumejipanga kushirikiana na TPDC kuanzisha mradi wa majaribio kwa mikoa ya Pwani na Lindi ambapo tutajenga mifumo ya mabomba yatakayopeleka gesi mpaka majumbani ili wananchi waanze kutumia gesi asilia ambayo inazalishwa hapa nchini na TPDC ndio wataisambaza gesi hiyo”, alisema Mhandisi Said
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.