SERIKALI imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanafanikiwa kushiriki zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Mafuguli katika hali ya utulivu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge nje ya uwanja wa Bunge la Tanzania.
Dkt. Mahenge amesema kuwa katika kurahisisha zoezi la kuuaga mwili ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli utapita katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma ili wananchi wengi waweze kushiriki katika tukio la kumuaga kiongozi wao.
Mkuu huyo wa Mkoa alizitaja barabara za mitaa utakapopita mwili la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ni kuanzia uwanja wa Jamhuri, “round about ya Bahi, uelekeo wa barabara ya Iringa, eneo la Mirembe, barabara ipitayo baa ya Kito kuelekea ‘Central’ Polisi, Jamatini, barabara ya kwenda Bunge, Mzunguko wa Shabiby, EMMAUS mataa ya kwenda kwa Waziri Mkuu, AfricaN Dreams, kutokea Wajenzi, barabara ya Arusha, kuelekea Airport.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba wakazi wa Dodoma kutokuwa na taharuki. “Tunaomba watu wasiwe na taharuki. Kila mtu atapata fursa ya kumuaga mpendwa wake. Tunawashukuru watu wote waliojitokeza jana barabarani kuelekea Ikulu ya Chamwino kumuaga Hayati Dkt. John Pombe Magufuli” amesema Dkt. Mahenge.
Awali katika uwanja wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu, kassim Majaliwa alisema kuwa katika kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa ya kumuaga Hayati Dkt. John pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa, mwili utazungushwa katika gari uwanjani hapo mara kadhaa ili wananchi wote wapate fursa ya kuaga mwili wa mpendwa wao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.