SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limeweka wazi kuwa linatarajia kuanza safafi za ndege za muunganiko kati ya Dodoma na Mwanza na Zanzibar na Pemba hivi karibuni.
Hayo yamesemwa leo tarehe 8 Oktoba 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mapokezi ya ndege mbili mpya aina ya Airbus A220-300 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi.
Mhandisi Matindi amesema tarehe 29 Julai 2021 Serikali ilisaini mikataba ya ununuzi wa ndege tano mpya kwa ajili ya kuongeza mtandao wa safari na kuboresha utoaji huduma wa Shirika la Ndege la Tanzania. "ATCL iko katika hatua za mwisho kuanzisha safari za muunganiko kati ya Dodoma na Mwanza na Zanzibar na Pemba" amefafanua zaidi Matindi.
Aidha, amesema kuwa safari za kimataifa zinazotarajiwa kuanzishwa kwa vituo vipya ni pamoja na Lubumbashi - DR Congo, Nairobi - Kenya na Ndola - Zambia. "Tunaendelea kufanya tathmini ya kuanzisha safari kati ya Dar es Salaam na Lagos Nigeria".
Akielezea kuhusu ndege zilizowasiri amesema kuwa "Ndege zetu zimeletwa na marubani wetu wenyewe na waandisi na wote waliohusika katika makabidhiano na ukaguzi wa ndege wote ni watanzania tofauti na miaka iliyopita. Ndege hizi mbili zilizokuja leo ni toleo jipya ambalo tumeboresha baadhi ya vitu kutokana na mahitaji katika soko na zitatuweka katika hali nzuri ya ushindani". Amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.