Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SHULE ya sekondari Itega imekamilisha ujenzi wa madarasa mawili kwa shilingi 40,000,000 fedha za mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira salama.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa shule ya sekondari Itega, Mwalimu Brighton Bwatota wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ya shule hiyo kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma mwisho wa wiki.
Mwalimu Bwatota alisema kuwa shule yake ilipokea fedha shilingi 40,000,000 mpato ya ndani ya jiji tarehe 13.10.2021 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili. “Ujenzi ulianza mwezi Novemba, 2021 kwa kutumia ‘force account’, kwa sasa ujenzi umekamilika na wanafunzi wanatumia madarasa hayo. Matumizi ya fedha shilingi 8,000,000 zilitumika kumlipa fundi na shilingi 32,000,000 zilitumika kununua vifaa vya ujenzi. Aidha, wakati wa utekelezaji wa mradi huu changamoto ilikuwa ni kupanda kwa gharama za za vifaa vya ujenzi na uhaba wa maji” alisema Mwalimu Bwatota.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Jaffar Mwanyemba alipoongoza kamati ya fedha na utawala ‘route one’ kutembelea na kukagua ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari Itega alipongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika katika kusimamia ujenzi wa madarasa hayo.
Ikumbumwe kuwa shule ya sekondari Itega ilianzishwa mwaka 2007, sasa ina wanafunzi 738 kati yao wavulana ni 312 na wasichana ni 426 ikiwa na walimu 44.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.