MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo ya utengenezaji wa vyungu vya kupandia na kuoteshea Maua kwa wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika kwa siku tatu katika bustani ya kikundi cha Kutunza Mazingira cha Chapakazi kilichopo Jijini Dodoma Barabara kuu iendayo Mkoani Iringa.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Eneo la kuoteshea Miche ya Miti na Maua linalomilikiwa na kikundi cha Chapakazi ambapo amewahimiza wanawake hao kuongeza ubunifu wa aina mbalimbali katika kuboresha bidhaa hizo pia ametoa wito kwa Taasisi za Serikali kupamba ofisi zao kwa kutumia vyungu vinavyotenezezwa na wanawake hao wanaomuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Nitoe wito kwa Taasisi zote za Serikali hakikisheni 10% ya mapambo ya ofisi zenu yanapambwa na vyungu vinavyotengenezwa na wanawake na Samia wa Mkoa wa Dodoma kwasababu wanawake Hawa Wana nia ya dhati ya kuwajulisha watanzania Mambo mbalimbali yanayoyofanywa na Rais wetu Dkt. Samia kupitia Kamati zao mbalimbali ikiwemo Kamati ya Mazingira", alisema Senyamule
Aidha, Senyamule amewaagiza wanawake hao kupitia Kamati ya Elimu kuendelea kuwahimiza wazazi na walezi wa watoto/ wanafunzi wa kidato cha kwanza kuhakikisha wanajiunga na kuanza masomo kwa wakati katika Shule walizopangiwa kujiunga nazo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.