Na. Coletha Charles, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simion Mayeka, ametoa wito kwa vijana wa Wilaya ya Dodoma kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kujihusisha na kampeni mbalimbali za kuleta tija na mabadiliko katika nchi kwa sababu ni nguzo ya taifa na mchango muhimu katika kufanikisha ndoto za maendeleo.
Mayeka alisema hayo wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) kwenye kilele cha mbio ndefu na fupi za Taasisi ya Anti-Corruption Voices Foundation yenye kauli mbiu ya Badili tabia Shepesha Rushwa katika shule ya msingi makole.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.