WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema, Serikali imendaa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) ambayo iko katika hatua ya mwisho ya mapitio inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Kairuki ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA).
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusu Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG), ulikuwa ni mfumo muhimu kwa ajili ya kupeleka fedha za maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali Mitaa (MSM) Tanzania Bara, kama nyenzo ya utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka sehemu ya fedha,"amefafanua Kairuki.
Pia amesema, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004/2005, mfumo huo ulichangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha, ulileta msukumo kwenye maeneo ya utendaji waMajukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo mipango, bajeti, usimamizi wa fedha pamoja na sekta nyingine kama Afya, Elimu, Maji na Kilimo.
"Mfumo wa LGDG ulikuwa mfano wa kuigwa kwa ufadhili wa uwekezaji wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha, kulikuwa na ongezeko la upatikanaji wa rasilimali fedha za maendeleo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na ndiyo ruzuku iliyowezesha kukamilisha maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
"Ndiyo ruzuku iliyotumika kuendesha ofisi na kujenga uwezo wa watendaji katika ngazi za kata,vijiji na mitaa na ndiyo fedha zilizotumika katika ufuatiliaji wa miradi kwa uhakika na kutekeleza miradi iliyoibuliwa na jamii,"alibainisha Kairuki.
Kairuki alisema, Mfumo wa LGDG ulihuishwa mwaka 2015/2016 na ulipaswa kuanza mwaka 2016/2017
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.