JARIDA maarufu la kibiashara duniani Forbes la nchini Marekani, limeitaja Hifadhi ya Taida ya Serengeti kuwa kivutio cha pili kwa kuvutia kutembelea zaidi watalii kwa mwaka 2021.
Forbes limesema kuwa Serengeti ina uhamiaji mkubwa zaidi wa wanyama duniani (largest terrestrial mammal migration in the world) kitu ambacho kimeifanya Serengeti kuwa moja kati ya maajabu saba ya asili barani Afrika na kuongeza kuwa ni sehemu ambayo mtalii ana bahati ya kuona aina mbalimbali za wanyama kwa muda mfupi.
Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti hutembelewa na zaidi ya watalii wasiopungua 350,000 kwa mwaka. Serengeti ina ukubwa wa kilometa za mraba 13,250 na inapatikana futi 3,737 hadi 7,133 kutoka usawa wa bahari. Vilevile mbuga hii ina misimu miwili mizuri ya kutembelea ambayo ni kipindi cha mwezi Juni hadi Julai na mwezi Januari hadi Februari.
Aidha jarida hilo limekitaja kisiwa cha Maldives kilichopo barani Asia kuwa ndicho kinachoshika nafasi ya kwanza kwa kuvutia watalii. Maldives imepewa nafasi hiyo kutokana na kuwa na mwonekano mzuri na maji yake kuwa safi.
Msafara unaokadiriwa kuwa na Nyumbu wanaohama milioni moja na nusu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.