SERIKALI imeanza mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni hatua ya awali ya benki hiyo kuangalia uwezekano wa kugharamia kwa njia ya mkopo wenye masharti nafuu ujenzi wa Bwawa la Farkwa ili kuwa chanzo kingine cha maji kwa Jiji la Dodoma na wilaya za Bahi, Chemba na Chamwino.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi za Wizara ya Maji zilizopo Mji wa Serikali Jijini Dodoma yakiwashirikisha Maafisa kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali kwa upande wake iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga aliyeongoza timu iliyojumuisha maafisa kutoka Wizara ya Maji, DUWASA na RUWASA.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.