Na. Tabitha Joshua, Dodoma
NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema serikali imeridhia kuboresha sekta ya kilimo kwa kutenga mashamba maalumu pamoja na mipango ya kuendeleza vijana kupitia kilimo ili kukuza uchumi na kupunguza idadi ya vijana tegemezi.
Kauli hii aliitoa kwenye kilele cha Maonesho ya Siku ya Wakulima (Nanenane) kwa Kanda ya Kati yaliyofanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania.
Katambi alisema “sekta ya kilimo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa taifa ambapo asilimia 80 ya watanzania wanategemea kilimo. Hivyo, serikali imeridhia kuboresha sekta hii ikiwa ni pamoja na kuzalisha mazao mbalimbali, kutenga mashamba maalum kwa mazao maalum, kununua mizani ya kupimia mazao, vifaa vya umwagiliaji na kuboresha mabwawa ya umwagiliaji”.
Akiongelea kaulimbiu ya maadhimisho ya Nanenane, 2023 inayosema “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu ya chakula” Katambi alisema kuwa vijana na wanawake wana mchango mkubwa sana katika sekta hii. Mchango wa uchumi unaotakana na shughuli za kilimo ni mkubwa mno hasa kwenye mifugo, uvuvi, pamoja na misitu ingawa ulishuka kwa 26.8% mwaka 2021 hadi 26.2% mwaka 2022 kutokana na ugonjwa wa Uviko-19.
Alimalizia kwa kusema kuwa serikali itaondoa urundikanaji wa kodi zisizo za lazima pia kuajili wataalamu wa sekta ya kilimo ili watumiaji waweze kupata bidhaa zinazoeleweka hivyo, kuwataka wakulima kuzalisha mazao kwa wingi na kuzingatia ubora wa mazao unaokidhi soko la kimataifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.