NAIBU Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati 300, hadi kufikia Februari 2023 kiasi cha shilingi bilioni 14.6 zimekwishatolewa.
Amesema hayo Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Wambura aliyetaka kujua Je, nini mpango wa Serikali kumaliza ujenzi wa Zahanati kwa vijiji vilivyokamilisha ujenzi wa maboma.
Dkt. Dugange amesema jumla ya zahanati 762 kati ya 1,514 ujenzi umekamilika na zimeanza kutoa huduma na ujenzi wa maboma 752 ya zahanati upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Aidha, Dkt. Dugange amesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2017/18 hadi 2021/22 kiasi cha shilingi bilioni 71.95 zimetolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 1,214 ya zahanati nchini kote.
Alisema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa kutenga bajeti ajili ya ukamilishaji wa maboma ya Zahanati yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.