WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inasimamia kikamilifu sekta ya nishati ikiwemo kuendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania ili kukuza uchumi.
“Mradi huu ni muhimu kwa manufaa ya nchi zetu mbili katika kukuza biashara, viwanda vya uzalishaji, kuongeza ajira pamoja na kuvutia wawekezaji ambao wanatarajia kukuza teknolojia na ujuzi kwa wananchi. Mheshimiwa Rais ana matamanio makubwa ya kuifanya sekta ya nishati kuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi na kuboresha sekta nyingine ikiwemo viwanda ambavyo ukuaji wake unategemea zaidi uwepo wa nishati ikiwemo mafuta na gesi.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2022) wakati akiahirisha mkutano wa nane wa Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. Amesema baadhi ya wadau wa maendeleo wamekuwa na mashaka katika utekelezaji wa mradi huo wakihofia kuwa unaweza kutekelezwa pasipo kuzingatia athari za kimazingira na haki za binadamu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.