Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Miloa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali inaridhishwa na utendaji wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo
kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kupitia mafunzo ya muda mrefu na mfupi, ushauri elekezi na tafiti katika nyanja za usimamizi na Menejimenti katika Serikali za Mitaa.
Mhe. Dkt. Dugange ameyasema hayo leo akimuwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati wa wa Mahafali ya 16 ya chuo hicho iliyofanyika Kampus kuu ya chup hicho iliyoko Hombolo jijini Dodoma.
Amesema jukumu hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda ya Serikali kuhusu Ugatuzi wa Madaraka (D by D)inayosisitiza upelekaji madaraka kwa wananchi hususani katika ngazi za msingi za Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.