NAIBU Katibu Mkuu anaeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amesema kuwa Serikali inatambua changamoto za Walimu zikiwemo upandaji wa madaraja,malimbikizo ya mishahara,malipo ya uhamisho pamoja malipo ya likizo.
Dkt. Msonde ameyasema hayo wakati akizungumza na Walimu katika eneo la Runzewe wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Amesema Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto zao na amewatoa hofu walimu wa eneo hilo kuwa Serikali italipa malimbikizo yao na waendelee kuchapa kazi.
Pia Dkt. Msonde amewataka maafisa elimu wa Msingi na Sekondari katika halmashzuri zote nchini kutotoa lugha zisizokuwa na staha kwa walimu.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi (Elimu) Dkt. Charles Msonde anatarajia kuendelea na ziara yake wilayani Chato na kuzungumza na walimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.