NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaid Ali Khamis, amesema dhamira ya Serikali ni kuendelea na jitihada za kuwalinda watoto wa kitanzania na kuwaondoa wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Tasker Restuta Mbogo Mbunge wa Viti Maalum, aliyetaka kujua jitihada za Serikali katika kukabiliana na ongezeko la watoto waishio na kufanya kazi mitaani na jitihada zinazochukuliwa na Serikali.
Akijibu swali hilo, Mwanaidi amesema kuwa, kuongezeka kwa watoto wa Mitaani kumetokana na sababu mbalimbali za kifamilia hali inayochangia watoto kukimbia kwenye kaya zao na kwenda kuishi na kufanya kazi mitaani na kuchochea kufanyika vitendo vya ukatili dhidi yao.
"Serikali inafanya jitihada na kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiweno kuimarishwa kwa Kamati za ulinzi wa Mama na Mtoto ndani ya Jamii, ambapo hadi hivi sasa kuna jumla ya Kamati 18,186,000 kwa ngazi ya Taifa lakini pia kutoa elimu kwa wazazi na walezi kupitia ajenda ya taifa ya uwajibikaji na malezi bora kwa watoto” amesema Mwanaidi.
Kuhusiana na zoezi la kuwaondoa watoto waishio Mitaani, amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau, inaendelea na zoezi la kuwabaini na kuwandoa watoto waishio Mitaani na kufanya kazi katika mazingira hatarishi.
aidha kwa upande wa watoto ambao walishindwa kutambuliwa kwenye kaya zao, Serikali imewachukua na kuwapeleka kwenye Makao ya watoto sambamba na kuwapatia huduma za Msingi kwenye Makazi ya Serikali na yale yanayomilikiwa na watu binafsi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.