RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika jukumu alilonalo la kuibeba Ajenda ya Nishati safi ya kupikia barani Afrika itawezesha kuhifadhi misitu na kulinda mazingira nchini.
Rais alisema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na washiriki wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Amewahimiza wanawake nchini Tanzania kutekeleza yatakayozungumzwa katika kongamano hilo na kuwaahidi serikali itaunga mkono yale yatakayotekelezwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Akifungua Kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alisema wakati Serikali inakamilisha taratibu za kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi, ni vema wadau mbalimbali kusaidia utekelezaji kupitia mikopo midogomidogo, vikoba au vikundi vya wanawake ili kuhakikisha wanwake wanapata vifaa vya nishati safi.
Aidha aliitaka Wizara ya Fedha kutazama uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia ili wananchi waweze kumudu kununua majiko hayo kwa urahisi. Makamu wa Rais amehimiza vijiji na watu binafsi wanaopata mapato kutokana na biashara ya kaboni kutumia mapato hayo kugharamia nishati safi ya kupikia.
Halikadhalika Makamu wa Rais alitoa wito kwa taasisi za utafiti, sekta binafsi na wadau wengine kubuni teknolojia rahisi na zitakazopatikana kwa gharama nafuu ili kuharakisha uhamaji kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu. Amesema teknolojia zinazohitajika ni pamoja na zile za kupata majiko yanayotumia nishati safi kuwezesha kupika chakula kinachoiva kwa muda mrefu kama maharage na kande badala ya kutumia mkaa au kuni
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.