SERIKALI ya awamu ya tano ina nia ya dhati ya kuboresha maeneo ya kutupia taka hususani madampo yaliyopo kwenye miji yawe ya kisasa.
Hayo yamesemwa na Dkt. Leonard Subi Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye kilele cha wiki ya usafi wa mazingira kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa na halmashauri iliyofanyika jijini Dodoma.
Dkt. Subi amesema kuwa uchafuzi wa mazingira utaokanao na taka ngumu umeendelea kuwa changomoto katika maeneo ya mijini.
“Ili kukabiliana na tatizo hili, Serikali imepanga kuongeza nguvu kwenye mamlaka za serikali za mitaa ili kuboresha miundombinu katika mitaa iliyopo nchini hasa katika suala la usimamizi wa taka ngumu na majitaka”.
Aidha, Dkt. Subi amesema serikali imeandaa mwongozo wa uwekezaji katika taka ngumu ili kuhamasisha uwekezaji na kuongeza jitihada za kuboresha usimamizi wa taka hapa nchini.
Hata hivyo alizitaka halmashauri hapa zipitie sheria ndogo za halmashauri ili kutekeleza vema sheria ya afya ya jamii yam waka 2009 hususani katika maeneo ya utiririshaji maji taka hasa katika maeneo ya mijini na kudhibiti tabia ya kujisaidia porini wakati wa kusafiri maarufu kama ‘kuchimba dawa’ ambayo bado imeendelea kuwepo.
Dkt. Subi aliwapongeza maafisa afya hao katka meneo ya ujenzi wa vyoo bora, unawaji mikono, huduma za afya mipaknai, udhibiti wa kipindupindu, Corona, mlipuko wa Dengue pmaoja na udhibiti wa taka zitokanazo na huduma za afya na mengine mengi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Afya Tanzania (CHAMATA) Twaha Mubarak ameishukuru Wizara ya afya kwa kufanya afya ya mazingira ni kipaumbele katika kuondoa magonjwa, hivyo wataalam wanajivunia na kuweza kupunguza ugonjwa wa Malaria na kufanikiwa kutimiza lengo la kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.