Serikali imeihakikishia Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na madawa ya kulevya kuwa itaendelea kuboresha huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya kupitia tiba ya Methodone.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga, Dkt. Leonard Subi, alipokuwa akijibu hoja za wabunge wa kamati hiyo inayoongozwa na Mhe. Oscar Mukasa walipofanya ziara kwenye kituo cha kuhudumia waathirika hao cha Itega, jijini Dodoma.
Amesema pamoja na kuwepo na kituo hicho pia Serikali inatarajia kufungua kitio cha Methodone mkoani Tanga mwezi Aprili mwaka huu.
Dkt. Subi amesema madawa ya kulevya ni vita ambayo inahitaji ushirikishaji wa sekta mbalimbali na ndio sababu wanatumia asasi zisizo za serikali ili kuwafikia watumiaji hao na kuwaleta kwenye vituo hivyo.
"Imesaidia sana kuwajenga kijamii na ndio maana kuna wengine wanasema ndoa ziliisha lakini kwa sasa wanaishi na wake zao" amesema Dkt. Subi.
Awali, akitoa taarifa ya kituo hicho, Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe na Kituo cha Itega, Dkt. Erasmus Mndeme, amesema waraibu hufika kituoni hapo kupitia asasi zisizo za serikali kama MEFADA, YOVARIE na YCR.
Amebainisha kuwa sasa kituo kina waraibu 479 ambapo 367 wanatumia dawa ya methodone kila siku. Ameeleza kuwa waraibu 26 wanaishi na Virui vya Ukimwi (VVU), wanne waligundulika na Kifuo Kikuu. Wengine 176 walipimwa homa ya ini ambapo 64 sawa na asilimia 36 waligundulika kuwa na homa ya ini aina ya B na C" amefafanua.
Dkt. Mndeme ameomba kamati hiyo kuwa mabalozi katika upatikanaji wa ajira na ushirikishwaji wa waraibu katika shughuli za kijamii ili wajiongezee kipato.
Naye, Meneja wa asasi isiyo ya kiserikali inayopambana na madawa ya kulevya (MEFADA), Alex Chitawala, amesema kuanzishwa kwa Kituo cha Itega kimeondoa kwenye mzunguko kiasi cha Sh. Bilioni 2.7 zililokuwa zikitumika na waraibu 367 kila mwaka kununua dawa za heroin.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na madawa ya kulevya walipotembelea Kituo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya kilichopo Itega jijini Dodoma.
Chanzo: wizara_afyatz (Intagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.