MRATIBU wa Mradi wa Programu ya uboreshaji wa elimu ya awali na msingi Boost kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Ally Swalehe amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 serikali imepata mafanikio makubwa ambapo jumla ya shule 302 zimejengwa vikiwemo vyumba vya madarasa madarasa 7230 na matundu ya vyoo yaliyojengwa ni 11297.
Akiongea kwenye ufunguzi wa mafunzo ya walimu wakuu na maafisa mazingira kuhusu miongozo ya ujenzi,usalama wa mazingira na jamii iliyofanyika Mkoani Morogoro. Swaleh amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025- 2025/2026 serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa 4770.
Anaenedelea kufafanua kuwa serikali imepanga kutekeleza mpango wa shule salama katika shule za msingi 6000 ambapo kwa mwaka 2023/2024 tayari serikali imetekeleza mpango huo katika shule za msingi 1000 na inategemea kwa mwaka 2024/2025 itaendelea na mpango huo kwenye shule 1500
Kuhusu kuuongeza uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi amesema Serikali imelenga kuongeza uandikishaji kutoka asilimi 79.6 iliyokuwepo mwaka 2021 hadi kufikia silimia 85 ifikapo mwisho wa programu 2025/2026 .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.