Na Nemes Michael, DODOMA
SERIKALI imesema itaendelea kulinda na kuhifadhi mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini pia kujielekeza katika matumizi ya nishati mbadala ili kuepuka athari za mazingira.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika ukumbi wa Hazina jijini hapa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka watumishi wa umma, wadau wa mazingira na vyombo vya Habari kuzingatia usafi na utunzaji wa mazingira siku zote bila kusubiri wakati wa maadhimisho.
“Tunapoazimisha wiki ya mazingira nasisitiza kuwa suala la hifadhi, utunzaji, usimamaizi na usafi wa mazingira lisiwe jambo linalofanywa wakati wa maadhimisho pekee, bali iwe ni suala la kila siku, kila siku iwe siku ya mazingira” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa alitoa wito kwa wakazi wa Dodoma ambapo takwimu zinaonyesha kuna matumizi makubwa ya kuni na mkaa kutokana na ongezeko kubwa la watu, kujielekeza zaidi katika matumizi ya nishati mbadala ili kuepuka athari za kimazingira.
Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa leo yatafanyika dunia nzima na yatafikia tamati tarehe 5 Juni, 2021.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.