NAIBU WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amesema Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa 'Sports and Arts Arena' katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam ikiwa na thamani ya jumla ya shilingi Bilioni 550 kwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau.
Gekul ameyasema Wizara yake imeshakamilisha hatua za awali za kutengeneza michoro ya Arena hizo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kibamba Mhe. Issa Jumanne Mtemvu aliyetaka kujua ni lini Serikali itajenga Sports Arena katika Wilaya ya Ubungo.
Mhe. Gekul ameongeza kuwa vikao vya mashauriano kati ya Wizara na Mkoa wa Dar es Salaam vinaendelea ili kukubaliana sehemu ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo eneno la Luguruini lililopo Manispaa ya Ubungo lenye ukubwa wa ekari 10.5 ni kati ya maeneo yanayotarajiwa kupendekezwa kwa ujenzi wa mradi huo na kwamba baada ya kukamilikika kwa hatua hizo ujenzi utaanza mara moja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.