Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SERIKALI kukabiliana na changamoto ya utoro kwa wanafunzi wanaotoka familia masikini kwa kuanzisha dirisha maalum kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF).
Kauli hiyo ilitolewa wakati wa kuwasilisha mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/2023 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema “Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameguswa sana na watoto kukatisha masomo kwa ajili ya sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu zinazosababisha kukatisha masomo ni umasikini wa kipato kwenye familia zetu, mimba za utotoni, mwamko duni wa elimu kwa baadhi ya jamii na utoro na wale wasioendelea kwa mujibu wa sheria (ufaulu). Ili kukabiliana na utoro wa wanafunzi wanaotoka familia masikini, bado tuna watoto wanaoshindwa kumudu mahitaji ya lazima licha ya kuwepo kwa programu ya elimu bila malipo na hivyo, wanasaidiwa na wabunge, madiwani na wengine kuchangiwa na wasamaria wema.
Napendekeza kuanzisha dirisha maalum kupitia TASAF litakalosaidia watoto wanaotokea familia masikini. Kwa msingi huo napendekeza kuanza na bilioni nane kwa ajili ya watoto masikini watakaopatikana kwenye kanzidata ya TASAF na taarifa za wabunge na madiwani”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.